Mark 12:35-37

35 aIsa alipokuwa akifundisha Hekaluni, akauliza, “Imekuwaje walimu wa sheria wanasema kwamba Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi?
36 cKwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, alisema: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’

37 dKwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?”

Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.

Isa Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Sheria

(Mathayo 23:1-36; Luka 20:45-47)

Copyright information for SwhKC